Proverbs 3

Faida Nyingine Za Hekima


1 aMwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

2 bkwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.


3 cUsiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe;
vifunge shingoni mwako,
viandike katika ubao wa moyo wako.

4 dNdipo utapata kibali na jina zuri
mbele za Mungu na mwanadamu.


5 eMtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

6 fkatika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.


7 gUsiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;
mche Bwana ukajiepushe na uovu.

8 hHii itakuletea afya mwilini mwako,
na mafuta kwenye mifupa yako.


9 iMheshimu Bwana kwa mali zako na
kwa malimbuko ya mazao yako yote;

10 jndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika,
viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.


11 kMwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana
na usichukie kukaripiwa naye,

12 lkwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,
kama vile baba afanyavyo
kwa mwana apendezwaye naye.


13 mHeri mtu yule aonaye hekima,
mtu yule apataye ufahamu,

14 nkwa maana hekima ana faida kuliko fedha
na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.

15 oHekima ana thamani kuliko marijani;
hakuna chochote unachokitamani
kinachoweza kulinganishwa naye.

16 pMaisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;
katika mkono wake wa kushoto
kuna utajiri na heshima.

17 qNjia zake zinapendeza,
mapito yake yote ni amani.

18 rYeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;
wale wamshikao watabarikiwa.


19 sKwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia,
kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;

20 tkwa maarifa yake vilindi viligawanywa,
nayo mawingu yanadondosha umande.


21 uMwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,
usiache vitoke machoni pako;

22 vndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako
na pambo la neema shingoni mwako.

23 Kisha utaenda katika njia yako salama,
wala mguu wako hautajikwaa;

24 wulalapo, hautaogopa;
ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.


25 xUsiogope maafa ya ghafula
au maangamizi yanayowapata waovu,

26 ykwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako
na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.


27 zUsizuie wema kwa wale wanaostahili
ikiwa katika uwezo wako kutenda.

28 aaUsimwambie jirani yako,
“Njoo baadaye, nitakupa kesho”:
wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.


29 abUsifanye hila ya kumdhuru jirani yako,
ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.

30 acUsimshtaki mtu bila sababu,
wakati hajakutenda dhara lolote.


31 adUsimwonee wivu mtu mwenye jeuri
wala kuchagua njia yake iwayo yote,

32 aekwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu,
lakini siri yake iko kwa mwenye haki.


33 afLaana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu,
lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.

34 agHuwadhihaki wale wanaodhihaki,
lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.

35 Wenye hekima hurithi heshima,
bali huwaaibisha wapumbavu.
Copyright information for SwhKC